SHIRIKA la kimataifa linaloshughulikia misaada la Medecins Sans Frontieres, limeonya kwamba vifo vitokanavyo na binadamu kung’atwa na nyoka huenda vikaongezeka duniani.
Hali hii inasababishwa na kuisha kwa akiba ya dawa zinazotibu sumu ya nyoka kuenea katika mwili wa binadamu aliyeng’atwa na nyoka wa aina mbalimbali.
Aidha taarifa zinaeleza kwamba jumla ya watu laki moja duniani hupoteza maisha kila mwaka kutokana na tatizo hilo ambalo limeanza kukithiri katika maeneo mengi.