NECTA YATAKA KUZIBWA KWA MIANYA YA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI YA DARASA LA SABA

NECTA YATAKA KUZIBWA KWA MIANYA YA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI YA DARASA LA SABA

Like
260
0
Tuesday, 08 September 2015
Local News

IKIWA imesalia siku moja kuanza kwa mitihani ya taifa ya darasa la saba, baraza la mitihani nchini –NECTA– limezitaka kamati za mikoa na wilaya kuhakikisha taratibu zote za mitihani zinazingatiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuzuia mianya inayoweza kusababisha udanganyifu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo, Katibu mtendaji wa baraza hilo Dokta Charles Msonde amesema baraza hilo halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakaye jihusisha na udanganyifu katika mitihani hiyo ikiwemo kuwafutia matokeo watahiniwa watakao bainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu.

Aidha Msonde ameongeza kuwa ni vyema kwa wananchi kuheshimu maeneo ya shule ambazo mitihani hiyo itafanyika ili kuhakikisha mitihani inafanyika kwa amani na utulivu kwakuwa elimu ya msingi ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Comments are closed.