MAELFU ya waandamanaji waliokuwa wakipeperusha bendera za Uturuki wamevamia makao makuu ya chama kikuu cha Kikurdi cha HDP.
Jengo hilo lililoko katika mji mkuu wa Ankara baada ya kuvamiwa lilichomwa moto.
Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amelaani vikali mashambulizi na uvamizi huo katika ofisi za kisiasa na hata kwa nyumba za habari na ametoa wito wa kusitisha ghasia.