KATIKA kuhakikisha kuwa inamshirikisha msikilizaji wake kwenye kila jambo na hatua inayopiga 93.7 efm, kupitia kipindi chake kipya cha Uhondo ambacho huruka hewani kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa Alasiri, Kikiwa na watangazaji mahiri Dina Marios na Swebe Santana (Rais wa Wanaume) kimeandaa shindano la Kanga kwa ajili ya wanawake wote wasikilizaji wa Efm.
Lengo la shindano hilo, linaloanza leo Septemba 14 na kuishia Oktoba 5 mwaka huu, kwanza ni kuwahamasisha wanawake wote wakione Kipindi cha Uhondo kuwa kimekuja kwa ajili yao, pili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia tatu kumwonyesha njia nyingine mwanamke itakayomkomboa badala ya kukaa nyumbani mwisho wa siku atajifunza ujasiriamali kupitia biashara ya Kanga.
Mfumo wa shindano lenyewe utakuwa kama ifuatavyo:
Wasikilizaji wa E fm ambao ni wanawake wanakaribishwa kushiriki shindano la kubuni maneno ya Kanga kupitia kipindi cha UHONDO na maneno hayo yawe na neno UHONDO . “Mfano Uhondo wa Ngoma uingie Ucheze” na Mshindi atajinyakulia kitita cha Shilingi za Kitanzania milioni moja.
Hata hivyo shindano hilo halitaishia hapo, kwani baada ya kupata mshindi neno lake la Ushindi zitatengenezwa kanga zitakazoandikwa neno hilo ikiwa ni hatua ya pili sasa ya kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi.
Zikishatengenezwa kanga hizo, Efm kupitia kipindi hicho cha Uhondo, itatatoa nafasi kwa wanawake kutengeneza pesa na kujikwamua kwa kuuza Kanga hizo na Mwanamke yoyote hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani atachukua kanga hizo na kuziuza ambapo kwa kila doti moja ya kanga atapata asilimia 30% ya pesa.
“ Ndugu zangu waandishi wa habari naomba kusisitiza tu hapa kuwa shindano hili litashirikisha wanawake pekee”. Alisema Dina Marios
Asanteni sana kunisikiliza.
IMETOLEWA NA
DINA MARIOS
MTANGAZAJI NA MTAYARISHAJI WA KIPINDI CH A UHONDO.
kushoto ni Afisa habari wa E-fm Lydia Moyo akifungua mkutano na waandishi wa habari, katikati ni Mkuu wa idara ya mawasiliano na mahusiano Dennis Ssebo na kulia ni Dina Marious mtangazaji wa kipindi cha Uhondo
Mkuu wa idara ya mawasiliano na mahusiano Dennis Ssebo akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni Afisa habari wa E-fm Lydia Moyo na kulia ni Dina Marious mtangazaji wa kipindi cha Uhondo
Dina Marious mtangazaji wa kipindi cha Uhondo akizungumza na waandishi wa habari juu ya shindano la Khanga la kipindi cha Uhondo
Dina Marious akielezea jambo