JUKWAA LA WAHARIRI LAWATAKA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NA MASHABIKI KUACHA KUSHAMBULIA WAANDISHI

JUKWAA LA WAHARIRI LAWATAKA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NA MASHABIKI KUACHA KUSHAMBULIA WAANDISHI

Like
315
0
Monday, 14 September 2015
Local News

IKIWA Zimepita siku tatu tangu kupigwa kwa Mwandishi wa habari wa magazeti ya Uhuru publications Limited UPL, CHRISTOPHER LISSA Katika ofisi za chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jukwaa la Wahariri Tanzania limewataka viongozi wa vyama vya siasa pamoja na mashabiki wa vyama hivyo kuacha vitendo vya kuwashambuliwa waandishi wa habari na kwamba vitendo hivi vikiendelea jukwaa litachukua hatua za kisheria dhidi ya vyama husika.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jukwaa hilo ABSALOM KIBANDA  amesema kuwa Jukwaa wamesikitishwa sana na kitendo hiko cha vijana wa CHADEMA Kuchukua sheria mikononi na kwamba tukio hili linaashiria kuwazuia waandishi wa habari kutekeleza wajibu wao wa msingi wa kukusanya taarifa na kuuhabarisha umma kuhusu mambo mbalimbali yanayo endelea nchini.

Comments are closed.