VIJANA WAMETAKIWA KUTOTEGEMEA KUAJIRIWA

VIJANA WAMETAKIWA KUTOTEGEMEA KUAJIRIWA

Like
197
0
Tuesday, 15 September 2015
Local News

VIJANA nchini wametakiwa kutumia vizuri mazingira yanayowazunguka katika kuibua mbinu mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kuondoka na Taifa tegemezi kwa kusubiri kuajiriwa mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Susan Ndunguru alipokuwa akifunga mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha yaliyofanyika Jijini Mwanza.

Ndunguru amesema kuwa vijana waliopata mafunzo ya uwezeshaji wa stadi za maisha ni mabalozi ambao wana uwezo mkubwa wa kuweza kujenga Taifa lenye Afya nzuri, weledi na ujuzi.

Comments are closed.