WIZARA YA MAMBO YA NJE YATOA UFANUNUZI WA SAFARI ZA RAIS KIKWETE NJE YA NCHI

WIZARA YA MAMBO YA NJE YATOA UFANUNUZI WA SAFARI ZA RAIS KIKWETE NJE YA NCHI

Like
256
0
Friday, 18 September 2015
Local News

Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa imesema kuwa imesikitishwa na taarifa zisizo za kweli zilizotolewa katika vyombo vya habari kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, katika kipindi cha miaka 10 ya uongozi wake ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano 5.

 

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inasema kuwa tangu Rais Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu wa nchi ambao ni Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki.

 

Wizara imeeleza kuwa kwa miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni 5 hadi 25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo na kuongeza kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara za viongozi.

Comments are closed.