WANANCHI MKURANGA KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA USAMBAZAJI MAJI

WANANCHI MKURANGA KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA USAMBAZAJI MAJI

Like
435
0
Friday, 18 September 2015
Local News

WANANCHI wa wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa usambazaji wa maji kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchimbaji wa kisima cha maji chenye urefu wa mita 541 ambacho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni  1.8  kwa siku.

 

Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima hicho  mwakilishi wa kampuni ya kuchimba visima ya ZENTAS  kutoka Uturuki nchini Tanzania dokta Mohammed Akbar amesema wanaendelea na majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini  jambo ambalo limeonesha mafanikio makubwa.

 

Dokta  Akbar amesema endapo maji hayo yataunganishwa kwenye miundombinu iliyopo katika mji huo yatakidhi mahitaji ya maji ya mji wa Mkuranga ambayo ni lita laki  Sita na Elfu mbili  kwa siku.

MK2 MK3

Comments are closed.