JAMII IMEOMBWA KUTUNZA NA KULINDA AMANI NA UTULIVU

JAMII IMEOMBWA KUTUNZA NA KULINDA AMANI NA UTULIVU

Like
345
0
Monday, 21 September 2015
Local News

JAMII hususani Vijana wameombwa kutunza, kulinda na kuendeleza amani na utulivu uliopo nchini kwa kutambua umuhimu wake na kutokubali kutumiwa na Mtu au Kikundi cha Mtu kuvuruga amani iliyopo.

Hayo yamesemwa leo katika Maadhimisho ya siku ya Amani duniani ambayo huazimishwa Septemba 21 kila mwaka na nchi zilizo katika Jumuiya ya madola ya umoja wa mataifa ambapo kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu ya “Ushirikiano wa amani, utu kwa wote” ikiwa na lengo la kuwaelimisha Vijana juu ya umuhimu wa kulinda na kujali amani ya nchi.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula amesema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inalinda Amani na kuheshimu demokrasia hasusani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu.

Comments are closed.