SERIKALI imeshauriwa kuboresha mishahara ya walimu ili waweze kufanya kazi kwa bidii tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa wakifanya kazi wakiwa na mawazo yakutojua kesho yao.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Rais wa chama cha ngumi Tanzania MUTTA RWAKALE wakati wa mahafali ya 12 darasa la saba shule ya msingi UKWAMANI ambapo amesema kuwa kutokana na walimu kuwa na mishahara midogo inaweza kuchangia kufeli kwa wanafunzi kutokana na kutokuwa makini wakati wakufundisha huku wakiwaza namna ya kupata fedha yakujitosheleza kimaisha.