WAMILIKI wa vitalu vya mbogamboga wametakiwa kufuata kanuni na taratibu za kiafya zilizowekwa na serikali pindi wanapolima kilimo hicho ili kulinda afya za watumiaji.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Ubungo NHC, AMANI SIZYA ameiambia efm radio kuwa asilimia kubwa ya wakulima wa mbogamboga wanatumia maji yanayopita kwenye mitaro ya maji taka kumwagilia mboga hizo, na kusababisha kutokuwa salama kiafya kwa watumiaji.