UINGEREZA imetangaza kwamba itawatuma wanajeshi wake Somalia kusaidia wanajeshi wanaolinda amani nchini humo.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema wanajeshi 70 watatumwa Somalia kujiunga na kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachowasaidia wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanaokabiliana na wapiganaji wa al-Shabab.
Amedokeza pia kuwa wanajeshi takriban 300 watatumwa Sudan Kusini.