VIPIMO VYA MARADHI YA MOYO KUFANYIKA BURE MUHIMBILI LEO

VIPIMO VYA MARADHI YA MOYO KUFANYIKA BURE MUHIMBILI LEO

Like
370
0
Tuesday, 29 September 2015
Local News

LEO ni Siku ya Afya ya Moyo Duniani ambapo kila ifikapo September 29  ya kila mwaka Dunia nzima huadhimisha siku hiyo inayolenga kuijulisha jamii baadhi ya masuala mbalimbali yanayo husu afya ya Moyo.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana, jijini Dar es salaam daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini, TULIZO SHEMU SANGA amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi leo katika hospitali ya Taifa ya muhimbili ili kupima afya hiyo bure.

Aidha DKT TULIZO ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2012 unaonyesha robo tatu ya WATANZANIA wanaugua ugonjwa huo na zaidi ya watu milioni 17.3 wanapoteza maisha kila mwaka duniani kote kufuatia maradhi hayo ya moyo.

Comments are closed.