JWTZ YAKABIDHIWA JENGO LA KUFUNDISHIA WATAALAMU WA SAYANSI YA TIBA

JWTZ YAKABIDHIWA JENGO LA KUFUNDISHIA WATAALAMU WA SAYANSI YA TIBA

Like
319
0
Tuesday, 29 September 2015
Local News

JESHI la Wananchi wa Tanzania-JWTZ- leo limekabidhiwa Jengo litakalotumika kwa ajili ya Chuo cha Kijeshi cha kufundishia wataalamu wa Sayansi ya Tiba kwa kiwango cha Shahada lililojengwa kwa msaada na Serikali ya Ujerumani ili kuongeza idadi ya Madaktari Nchini.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Ulinzi Dokta Hussen Mwinyi amesema awali Jeshi hilo lilikuwa na chuo kinachofundisha matabibu kwa kiwango cha Cheti na Stashahada hivyo chuo hicho kitaweza kutoa elimu hiyo kwa kiwango cha kinachotakiwa.

Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani Nchini Egon Kochanke akimwakilisha Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani amesema  Jeshi la Wananchi waTanzania  ni miongoni mwa Majeshi yenye uhusiano wa karibu na Jeshi la Ujerumani hivyo katika kudumisha uhusiano huo Ujerumani itaendelea kutoa msaada katika sekta mbalimbali hususani masuala ya afya.

Comments are closed.