BODI ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imesema kuwa imeandaa miongozo ya utoaji huduma bora katika kufanikisha Mpango wa uwiano wa Itifaki ya pamoja kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa ZFDB Dokta Burhani Othman Simai ameeleza hayo katika Mkutano wa wadau wa dawa Zanzibar ulioandaliwa na Mpango wa Udhibiti wa bidhaa za Chakula na Dawa wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Katika mkutano huo dokta Simai amesema kuwa kuanzia sasa bidhaa zote za chakula na dawa za Zanzibar na zinazotoka nje zitasajiliwa na Bodi huku Viwanda vinavyotengeneza bidhaa hizo vitafanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha usalama wa bidhaa hizo.