IDADI ya watu waliouwawa katika shambulio la anga kwenye sherehe ya harusi nchini Yemen imefikia watu 131, na kuaminika kuwa shambulio hilo ni baya kuwahi kutokea katika vita nchini Yemen.
Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unafanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya waasi nchini Yemen umekanusha kuhusika na shambulio hilo huku msemaji wa muungano huo amesema wanamgambo wa eneo hilo huenda wameshambulia kwa makombora.
makombora hayo yaliyorushwa jana yameharibu mahema katika kijiji cha Al-Wahijah katika bahari ya Sham, karibu na mji wa bandari wa Al-Mokha ambapo mtu mmoja anayehusika na kundi la Wahuthi alikuwa akisherehekea harusi.