MACHAFUKO 15 WAUAWA BURUNDI

MACHAFUKO 15 WAUAWA BURUNDI

Like
228
0
Monday, 05 October 2015
Global News

WATU wapatao 15 wameuawa katika makabiliano kati ya waandamanaji na polisi kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura.

Kiongozi wa Baraza la Haki za Binaadamu la nchi hiyo, Anschaire Nikoyagize, ameliambia shirika la habari la Ujerumani, DPA, kwamba kulikuwa na milio ya risasi kwenye mitaa ya Mutakure na Cibitoke, na hadi wakati huo walishapata maiti 15, ingawa idadi ilitazamiwa kuongezeka.

Ghasia zimelikumba taifa hilo dogo la Afrika Mashariki, tangu Rais Pierre Nkurunziza kutangaza azma yake ya kuwania muhula wa tatu madarakani hapo mwezi Aprili, na baadaye kushinda uchaguzi wenye utata mwezi Julai mwaka huu.

Comments are closed.