MADEREVA WAGOMA MOROGORO

MADEREVA WAGOMA MOROGORO

Like
299
0
Monday, 05 October 2015
Local News

WAKAZI wa Manispaa ya Morogoro leo wamelazimika kutembea kwa miguu   na wengine kutumia magari ya mizigo pamoja na pikipiki kwenda kazini huku wanafunzi wakibaki katika vituo vya daladala baada ya madereva kugoma  wakishinikiza jeshi la polisi kuwaachia huru baadhi ya madereva wanaoshikiliwa  kwa siku sita  mfululizo kutokana na makosa ya usalama barabarani.

 

Wakizungumza na Efm, katika vituo mbalimbali vya daladala mkoani humo,  wakiwemo wanafunzi na wanachi waliokwama kufika sehemu mbalimbali wamelalamikia serikali kushindwa kudhibiti mambo kama hayo ambayo yanaleta kero na usumbufu kwa raia  ambapo mgomo huo umeathiri mambo mengi ikiwa ni pamoja na wanafunzi  wa sekondari waliokuwa kwenye mitihani ya majaribio.

Comments are closed.