IMEELEZWA kuwa uwepo wa mfumo mpya wa utoaji leseni kupitia mtandao itawezesha kupunguza adha kubwa iliyokuwa ikikwamisha utoaji wa leseni kwa kipindi kirefu.
Akizungumzia mfumo wa zamani Kamishna wa Madini nchini Mhandisi Paul Masanja amesema kuwa mfumo huo ulikuwa na changamoto nyingi kwa kuwa ulitegemea umahiri na uadilifu wa Afisa anayeshughulikia leseni hali iliyosababisha baadhi ya Waombaji kukosa leseni bila sababu za msingi.
Kamishna Masanja ameongeza kwamba licha ya changamoto walizozipata waombaji wa leseni, Wizara pia ilikuwa na wakati mgumu wa kuhakikisha inatatua changamoto hizo kwani maombi ya wakati huo yalikuwa yakifanywa kwa kutumia karatasi.