ZAIDI ya watu 60 wamefariki kufuatia kulipuka kwa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari katika jimbo la mashariki la Diyala nchini Iraq.
Shambulio lingine la bomu limetokea katika mji wa kusini mwa Barsa ambao kwa kipindi kirefu haujakumbwa na mashambulizi ya mabomu huku maafisa usalama nchini humo wakisema bomu hilo lililotegwa katika mtaa wa Zubair limeua watu kumi.
Hata hivyo kundi la kiislamu la –IS- limethibitisha kuhusika katika mashambulizi hayo.