BALOZI OMBENI SEFUE KUFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA TAKWIMU

BALOZI OMBENI SEFUE KUFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA TAKWIMU

Like
279
0
Thursday, 08 October 2015
Local News

KATIBU mkuu kiongozi balozi ombeni sefue leo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa wadau wa takwimu ulioandaliwa na ofisi ya taifa ya takwimu (nbs) kwa ajili ya kukubaliana jinsi ya kushirikiana katika kuhakikisha takwimu za viashiria vya mpango wa maendeleo endelevu zinapatikana kwa wakati.
akizungumza na wandishi wa habari jijini dar es salaam jana  afisa habari wa ofisi hiyo, veronica kazimoto amesema mkutano huo utakuwa na lengo la kuelimishana juu ya kukamilika kwa utekelezaji wa malengo ya milenia (mdgs) na kuanza kwa malengo mapya ya maendeleo endelevu (sdgs).

 

kazimoto amefafanua kuwa mkutano huo utahudhuriwa na wadau wa takwimu takribani 100 kutoka wizara, idara, wakala na taasisi za serikali, wadau wa maendeleo pamoja na wadau wa taasisi za elimu ya juu.

Comments are closed.