WAKAZI wa jiji la Dar es salaam wamewaomba wamiliki wa vyombo vya usafiri kuangalia upya viwango vya bei ya nauli mara baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA kushusha bei ya mafuta .
Wakizungumza na E fm baadhi ya wakazi hao wamewaomba wamiliki kuwapunguzia bei za nauli kwani bei za mafuta zimeshuka kutoka bei za awali ambapo zilikuwa shilingi 2300 kwa lita moja ya petroli tofauti na ilivyo sasa ambapo bei ya petrol kwa lita moja ni shilingi 2000 na senti 86.
Naye mmoja wa watendaji wa chama cha wamiliki wa mabasi nchini-TABOA, Mbazi Mbazi amesema kuwa mchakato wa ushukaji wa nauli unategemea mambo mengi hivyo kushuka kwa mafuta siyo kigezo pekee kinachochangia kushuka kwa nauli.