MAWAZIRI wa ulinzi wa Jumuiya ya kujihami ya Nato leo wanajiandaa kujadili iwapo waimarishe ulinzi wa kanda ya kusini ya ushirika huo wa kijeshi, kutokana na wasiwasi nchini Syria, baada ya kujiingiza kwa Urusi katika mgogoro huo hivi karibuni.
Kabla ya mkutano huo mjini Brussels, Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema makanda wa kijeshi wamethibitisha kwamba jumuiya hiyo inauwezo na miundo mbinu inayohitajika kuliweka jeshi lake upande wa kusini na kubakia eneo hilo.