TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC– imewaasa wapiga kura kote nchini kuhakiki taarifa zao katika vituo vya kupigia kura siku nane kabla ya uchaguzi.
Hayo yamesema jana na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva alipokuwa akizungumza katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo Jaji Mstaafu Lubuva amewasihi viongozi hao kunadi sera zao majukwaani na sio kuilalamikia Tume katika majukwaa wakati wa kampeni pia amewataka wanasiasa hao kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika na kuacha kukimbilia kutoa taarifa zisizo za kweli kwa waandishi wa habari.