RAIS wa Marekani, Barack Obama ametangaza kuwa vikosi vya marekani vyenye silaha vimepelekwa Cameroon kusaidia mapambano dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram.
Kikosi cha wanajeshi 300, kitafanya operesheni za upelelezi, kijasusi na operesheni za kipelelezi katika ukanda mzima.
Cameroon na Chad zimekuwa zikilengwa na wanamgambo hao kutoka kaskazini mwa Nigeria na Obama amesema vikosi hivyo vitaendelea kubaki Cameroon mpaka watakapokuwa hawahitajiki tena.