93.7 EFM inaendeleza burudani kupitia kampeni yake ya muziki mnene bar
kwa bar. Jumamosi ilikuwa zamu ya wakazi wa bunju kuongea na muziki wa
93.7 EFM.
Burudani hiyo iliendeshwa na timu nzima ya EFM, iliyocheza mechi na
carlfonia FC ya boko na kuwafunga magoli mawili kwa moja katika uwanja
wao wa nyumbani uliopo ndani ya shule ya msingi boko. “Kwa bahati mbaya
tumeshafungwa mechi tatu ila kuanzia mechi hii ni mwendo wakufunga magori
ya kishujaa” alisema Dennis Ssebo mkuu wa idara ya mahusiano na
mawasiliano.
Baada ya mechi hiyo shangwe ziliendelea ndani Rainer park boko huku Rdjs wa
93.7 Efm wakitoa burudani ya aina yake iliyo acha historia kwa wakazi wa
boko.
Rdj X5 na Rdj timber wakifanya kazi yao kwa umakini.