KAMATI ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania –TCRA imetoa rai kwa vyombo vya utangazaji nchini kuendelea kutangaza habari zenye kudumisha amani ya watanzania kwa siku hizi chache zilizo baki kuhitimisha zoezi la upigaji kura.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo Bi MARGARET MUNYANGI wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa vituo vya utangazaji katika kutangaza habari za kampeni za vyama vya siasa kupitia vituo vyao.