KITENGO cha upasuaji wa moyo Mhimbili, kimetangaza kujitenga kutoka kwenye kitengo na kuwa Taasisi inayojitegemea kwa lengo la kuboresha huduma zake na kuwa taasisi ya kisasa kwa Afrika Mashariki ikitatambulika kama Taasisi ya moyo ya JAKAYA KIKWETE.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam, wakati wa kutangaza mabadiliko hayo Kaimu mkuu wa taasisi hiyo Profesa MOHAMEDI JANABI amesema kuwa mbali na kujitenga huko pia taasisi hiyo imekuwa na mafaniko makubwa ambapo mwaka huu pekee 2015 wameweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 172 ikilinganishwa na kipindi cha miaka sita iliyopita kutoka mwaka 2008 hadi mwaka 2014 waliwezea kufanya upasuaji wawagonjwa 394 pekee.