KESI ya Kikatiba kuhusu tafsiri ya Umbali wanaotakiwa kusimama wapiga kura baada ya Kupiga kura Wakati wa Uchaguzi mkuu inasomwa leo na kutolewa maelekezo maalum baada ya hapo jana kuahirishwa.
Akizungumza jana wakati anatoa maamuzi hayo mwenyekiti wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo JAJI SAKIETI KIHIYO ameleza kuwa baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili kuhusiana kesi hiyo jana, mahakama imetoa uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo watatoa maamuzi yenye maelekezo maalum kuhusu umbali ambao wapiga kura watatakiwa wakae baada ya kupiga kura siku ya Uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu.