ASASI YA AGENDA YATOA WITO KUTOLEWA KWA ELIMU YA MADHARA YA MADINI YA RISASI

ASASI YA AGENDA YATOA WITO KUTOLEWA KWA ELIMU YA MADHARA YA MADINI YA RISASI

Like
266
0
Tuesday, 27 October 2015
Local News

ASASI isiyo ya kiserikali ya AGENDA imetoa wito kwa serikali na wadau wengine kuelimisha jamii juu ya madhara ya madini ya risasi na jinsi ya kuyaepuka kwani yanaathari kubwa kwa watoto na mama wajawazito.

Akizungumza na waandfishi wa habari jijini Dar es salaam katibu mtendaji wa Asasi hiyo Silvani Mng’anya amesema kuwa katika wiki ya kukuza uelewa kwa jamii kuhusu athari za madini ya risasi wananchi wanatakiwa kujua kuwa madini hayo yanaathiri mfumo wa mwili wa binadamu ikiwemo ubongo, moyo na figo.

MNG’ANYA ameongeza kuwa kuelimisha jamii kutasaidia kuhamasisha uthibitishaji huria wa viwango vya madini ya risasi nchini ambapo kutachangia kutumika kwa viwango vinavyotakiwa katika rangi za mafuta.

 

Comments are closed.