CHAMA cha kihafidhina nchini Poland cha sheria na haki PiS kimeshinda uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa jana jumatatu.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi zinasema kuwa Chama cha PiS kilipata asilimia 37.6 ya kura, huku chama cha Civic Platform PO kimeshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 24.1.
Mgawanyiko rasmi wa viti bungeni ulikuwa bado haujapatikana, lakini wadadisi wanasema matokeo huenda yakatoa kwa chama cha PiS, ukiwa ni ushindi mkubwa kwa chama kimoja tangu Poland kuachana na siasa za kikomunist mwaka 1989.