HOFU YA KIPINDUPINDU YATANDA MBEYA

HOFU YA KIPINDUPINDU YATANDA MBEYA

Like
422
0
Friday, 06 November 2015
Local News

WAKAZI wa jiji la Mbeya wameingiwa na hofu ya kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu kutokana na mlundikano wa taka katika maeneo yao.

 

Wakazi hao wameingiwa na hofu hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho mvua inanyeesha na takataka bado zimeendelea kuwepo katika ghuba la kuhifadhia taka kwa muda mrefu.

 

Akiongelea malalamiko hayo ya wananchi Afisa Afya wa jiji la Mbeya Daktari JOHNSON NDARO amesema wameshindwa kuondoa taka katika makazi ya watu kutokana na ubovu wa magari pamoja na ukosefu wa fedha. Hata hivyo  Dokta NDARO amesema Halmashauri ya jiji la MBEYA inaendelea na jitihada za kutengeneza magari hayo ili waweze kuondoa taka hizo.

Comments are closed.