BARAZA la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC kwa kushirikiana na jeshi la kujenga taifa JKT limeanzisha program ya kutoa mafunzo ya mtaala maalumu kwa ajili ujasiriamali na uendeshaji wa biashara kwa vijana wanaojiunga na jeshi hilo kwa kujitolea.
Vijana hao ambao hawapati ajira wanafikia elfu 2,hivyo NEEC imeamua kuwaendeleza kutokana na mafunzo ya elimu za stadi za maisha wanayopata wawapo jeshini kwa kipindi chote cha miaka miwili .