MJUMBE wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ambaye anaondoka ameyataka makundi hasimu nchini humo kusitisha juhudi zao za kuzuwia mpango wa kugawana madaraka unaolenga katika kumaliza mzozo wa kisiasa nchini mwao.
Bernardino Leon, ambaye nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa hivi karibuni na mwanadiplomasia wa siku nyingi wa Ujerumani, Martin Kobler, pia amejitetea dhidi ya maelezo kwamba kuna mvutano wa kimaslahi kwake kukubali kazi katika Umoja wa Falme za Kiarabu kuwapa mafunzo wanadiplomasia kutoka moja kati ya mataifa ya Kiarabu ambayo inahusika sana na mzozo wa Libya.