KIONGOZI wa upinzani nchini Myanmar Bi. Suu Kyi amesema kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita nchini humo haukuwa huru lakini ulikuwa wa haki.
Kwenye mahojiano ya kipekee, Bi Suu Kyi aliwapongeza wananchi wa Myanmar kwa kumpigia kura ingawa Chini ya katiba ya nchi hiyo hawezi akawa rais, lakini amesema kwamba kama kiongozi wa chama atamteua rais.
Uchaguz huo umechukuliwa na wengi kuwa ndio wa kidemokrasia zaidi katika kipindi cha miaka 25, baada ya miongo kadhaa ya uongozi wa kijeshi.