WAKAZI wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali baadhi ya watumishi wa Idara ya Ardhi kwenye halmashauri ya mji wa Babati kwani wamehusika kusababisha migogoro ya ardhi wilayani humo.
Wakazi hao pia wameeleza kuwa, migogoro mingi ya Ardhi kwenye wilaya hiyo imesababishwa na baadhi ya watumishi wasiokuwa na maadili na wanaojali maslahi yao binafsi badala ya kujali maslahi ya wananchi.
Kwa upande wakes mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela amesema atahakikisha anasimamia vyema sheria ili mtumishi yeyote wa Idara ya Ardhi ambaye ataleta uzembe anachukuliwa hatua kali za kisheria.