MAREKANI imeiondolea Liberia vikwazo vya kiuchumi huku Rais Barack Obama akiipongeza nchi hiyo kwa kujitolea kufanikisha demokrasia tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003.
Vikwazo hivyo viliwekwa miaka 11 iliyopita dhidi ya kiongozi wa wakati huo Charles Talyor ambaye kwa sasa yupo gerezani kwa makosa ya uhalifu wa kivita.
Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, Rais Obama amesema kwa kuwa utawala wa Taylor ulimalizika na tayari kwa sasa yupo gerezani ina maana kwamba vikwazo hivyo havihitajiki tena.