UFARANSA imefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu katika mji wa Raqqa, nchini Syria.
Mashambulizi hayo ya anga ni ya kwanza kufanywa na Ufaransa tangu mji wake mkuu, Paris, kushambuliwa usiku wa Ijumaa na kundi hilo, ambapo watu 132 waliuawa.
Maafisa wa Ufaransa wamesema mabomu 20 yaliangushwa na ndege zaidi ya kumi, zilizoruka kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu na Jordan, kwa kushirikiana na kituo cha kijeshi cha Marekani.