Muingereza Andy Murray anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani ameanza vema michuano ya dunia ya tenesi kwa ushindi.
Murray alimshinda mpinzani wake David Ferrer, wa Hispania, ambae anashikia nafasi ya saba kwa ubora wa mchezo wa tenesi kwa jumla ya seti 6-4 6-4.
Nae Rafael Nadal, akamchapa Stan Wawrinka kwa jumla ya seti 6-3 na 6-2, hivyo Nadal kulipa kisasi cha kufungwa na Wawrinka katika michuano ya Paris Masters, mchezo huu ulitumia muda wa saa moja na dakika 23.
Kwa ushindi wa nyota hawa wiwili watachuana katika mchezo unaofuata wa michuano hiyo ya dunia hapo kesho jumatano.
Iwapo Murray atashinda mchezo huo atajihakikishia kuwa namba mbili katika ubora wa viwango vya ubora vya mchezo kwa mwaka 2015.