USHIRIKIANAO mdogo kati ya wazazi, walimu na wanafunzi mkoani TABORA umetajwa kuwa ni sehemu ya vikwazo vya kimaendeleo ya elimu ya msingi mkoani humo.
Hayo yamebainishwa na wadau mbalimbali wa elimu mkoani TABORA walioshiriki mdahalo wa masuala ya elimu uliohoji anguko la elimu mkoani humo.
Moja ya vitendo vilivyotajwa kufanywa na wazazi ni pamoja na kuwepo kwa hisia za vitendo vya kishirikina hali inayotajwa kukimbiza walimu wengi wanaopangwa kufundisha shule za msingi mkoani humo.