CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA MITAJI YAWAKABILI WASINDIKAJI WADOGO WA MAFUTA YA MBEGU YA ALIZETI

CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA MITAJI YAWAKABILI WASINDIKAJI WADOGO WA MAFUTA YA MBEGU YA ALIZETI

Like
338
0
Monday, 23 November 2015
Local News

KUTORATIBIWA kwa mbegu za Alizeti na ukosefu wa mitaji umeelezwa kuwa changamoto kubwa kwa wasindikaji wadogo wa mafuta ya mbegu ya alizeti katika uendeshaji wa viwanda.

 

Hayo yameelezwa na Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO) Vedastus Timothy wakati akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez.

 

Timothy amesema kwamba pamoja na kuwepo kwa taarifa za mbegu za kutosha nchini lakini hali inayoelezwa na wasindikaji inaashiria kwamba sekta hiyo hairatibiwi vyema kwani wasindikaji hukaa muda mrefu bila kuwa na mbegu za kusindika.

Comments are closed.