MGOMBEA Urais kupitia chama cha upinzani cha Conservative Mauricio Macri amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Argentina huku mgombea wa chama tawala akikubali kushindwa.
Matokeo yaliyotangazwa yameonesha Macri amepata asilimia 52 ya kura zote zilizopigwa huku mgombea wa chama Tawala Daniel Scioli akipata asilimia 48.
Hata hivyo katika Uchaguzi wa awamu ya kwanza uliofanyika mwezi Oktoba Macri ambaye ni meya wa zamani wa Buenos Aires, alikuwa ameshindwa na Scioli ambaye ni gavana wa mkoa wa Buenos Aires.