HATIMAYE Makontena tisa yalio kamatwa jana maeneo ya mbezi tangi bovu mali ya kampuni ya HERITAGE EMPIRE COMPANY LIMITED yamefunguliwa na kukaguliwa na kukutwa na malighafi za ujenzi wa kiwanda.
Makontena hayo tisa ambayo yana milikiwa na kampuni ya HERITAGE EMPIRE yameanza kukaguliwa toka jana jioni na kukamilika leo ambapo e fm imeshuhudia ukaguzi huo na kukuta malighafi mbalimbali za ujenzi kama vile vyuma vikubwa vyenye uwezo wa kujenga kiwanda cha ukubwa wa square mita za mraba elfu nne vitu vingine vilivyo kutwa ni mabati na vifaa maalumu kwa ajili ya kupoza na kuruhusu hewa kuingia kwenye majengo ya viwanda GLASS WOOL