SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema haina mpango wa kufunga maduka ya dawa baridi yaliyopo katika maeneo ya Hospitali za Serikali ispokuwa mpango waliokuwa nao ni kuhakikisha kuwa wanaimarisha upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu pamoja na kuboresha huduma muhimu ziweze kupatikana kwa ubora na haraka zaidi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Donan Mmbando wakati wa ziara yake ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuangalia namna utekelezaji wa Agizo la Rais Magufuli unavyoenda kufuatia Serikali kuagiza kufunguliwa kwa duka la dawa katika Hospitali hiyo kutokana na kuwepo na ukosefu mkubwa wa dawa katika Hospitali hiyo.