MFUKO wa afya ya jamii umezindua rasmi huduma ya tiba (TIKA) kwa kadi katika Manispaa ya Temeke utakao mwezesha mwananchi kupata hudua hiyo kwa gharama nafuu.
Akizungumza katika ufunguzi huo, mkurugenzi wa mfuko wa afya ja jamii – CHF, bwana Eugen Mikongoti amesema kuwa mpango huo ni mpango wa hiari ulioanzishwa kwa sheria namba 1 ya mwaka 2001 ambapo chini ya mpango huo mwana jamii anaweza kuchangia kiasi cha fedha kilicho kubalika katika mamlaka ya jamii ili kumwezesha kupata matibabu kwa mwaka mzima .
Aidha amefafanua kuwa mwana chama wa TIKA atapata huduma zote za afya ikiwemo huduma ya wagonjwa wa kutwa na kulazwa huduma za upasuaji kulingana na taratibu zilizo wekwa, Pamoja na huduma za rufaa pale zinapo hitajika.