TAASISI isiyo ya kiserikali ya- NEMA FOUNDATION imetoa msaada wa mashuka miamoja katika baadhi ya hospitali za Jijini Dar es salaam ikiwemo hospitali ya Mwananyamara ikiwa ni sehemu ya utaratibu wao ambao wanaufanya kila mwaka.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bi Mariam Dedes amesema kuwa wameguswa kutoa misaada hiyo kwa kutambua changamoto mabalimbali zinazo ikabili sekta ya Afya.
Kwa upande wake Mbunge wa kinondoni Muheshimiwa Mahulid Mtulya ameishukuru taasisi hiyo na kuziomba taasisi nyingine kujitokeza kutoa misaada kwenye hospitali hiyo kwani bado inakabiliwa na changamoto nyingi.