WAKAZI wa mtaa wa Ibanda kata ya kirumba Jijini Mwanza wanatarajiwa kupokea mradi wa uwekaji Alama katika maeneo yao ili kupunguza migogoro ya Ardhi iliyokithiri katika kata yao.
Hayo yamekuja mara baada ya mtaa huo kuwa na migogoro ya ardhi ya mara kwa mara na kuwaathiri wananchi waishio katika maeneo hayo.
Mwenyekiti wa mtaa huo Ephrahim Nkingwa amesema tayari amewasilisha barua kwa mkurugenzi wa Jiji ya kuomba upimaji shirikishi ili kuhakikisha maeneo yote ya mtaa huo yanapimwa na kuepusha migogoro hiyo.