RAIS Xi Jinping wa China na Barack Obama wa Marekani walikuwa na mazungumzo ya simu leo na kuahidi kwamba nchi zao zitaendelea kushirikiana katika suala la mabadiliko ya tabia nchi.
Televisheni ya taifa nchini China imeripoti kwamba marais hao wawili wamesema watashirikiana kwa karibu kuendeleza mafanikio yatakayotokana na mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabia nchi unaoendelea mjini Paris, Nchini Ufaransa.