IMEELEZWA kuwa Jimbo la Mbagala linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ajira kwa vijana pamoja na elimu ya ujasiliamali .
Mbunge wa Mbagala Issa Ali Mangungu kupitia chama cha mapinduzi -ccm- ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza katika mahafali ya kituo cha elimu na mafunzo ya afya –KEWOVAC-
Amesema kuwa wilaya nzima ya Temeke kuna chuo kimoja tu cha ufundi hali inayosababisha vijana wengi kushindwa kupata ujuzi ambao utawakwamua kiuchumi na badala yake huishia vijiweni.