IMEELEZWA kuwa, ili kuhakikisha kwamba wananchi wanaishi kwa raha na amani kipindi chote cha mwaka hasa kipindi cha masika, serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania leo imeanza kubomoa baadhi ya maeneo yanayo zunguka bonde la mto msimbazi.
Efm imetembelea maeneo ambapo zoezi la bomoa bomoa limetekelezwa na kushuhudia katapila la serikali likivunja nyumba hizo ambapo mpaka efm inaondoka zaidi ya nyumba 30 zilikuwa zimevunjwa .
Wakizungumza na e fm huku zoezi likiwa linaendelea baadhi ya viongozi wanao simamia zoezi hilo wamesema wao kama viongozi wamefika pale ili kukamilisha Zoezi ambayo walilitolea taarifa mapema kwa wakazi hao tangu mwaka ulio pita .